
Umahiri katika Historia ya Tanzania na Maadili ni kitabu kilichoandaliwa kwa kuzingatia
maudhui ya Muhtasari wa 2023 wa somo la Historia ya Tanzania na Maadili kwa
Kidato cha Kwanza. Uwasilishaji wa mada na dhana mbalimbali katika kitabu hiki
umezingatia ujenzi wa umahiri kama inavyopendekezwa katika mtaala wa elimu
ulioboreshwa. Kitabu kimehusisha vipengele vifuatavyo vinavyokifanya kiwe chaguo
sahihi kwa kila mwanafunzi wa somo la Historia ya Tanzania na Maadili:
• Bunguabongo kumsaidia mwanafunzi kutafakari kuhusu dhana mbalimbali za
kihistoria.
• Kazi za kufanya ili kumpa mwanafunzi nafasi ya kushiriki kikamilifu katika mchakato
mzima wa kujifunza historia na maadili ya taifa lake.
• Vielelezo vya kutosha kumsaidia mwanafunzi kuelewa kwa haraka zaidi dhana
zinazoelezewa katika kitabu.
• Visamafunzo kwa ajili ya kumpatia mwanafunzi mifano halisi ya dhana
zinazofundishwa darasani.
• Mazoezi ya marudio kila mwisho wa sura kumsaidia mwanafuzi kujipima kama
ameweza kupata umahiri uliokusudiwa katika sura husika.
• Majaribio mwishoni mwa kitabu ili kumjengea mwanafunzi uzoefu kuhusu mitihani
ya mwisho wa mwaka na ya kitaifa.
No reviews , Be the first to write a review
- ISBN : 9789912755338
- Publication Date : November 2024
- Language : Swahili
- Number of Pages : 209
- Cover Format : Paperpack
- Edition : First Edition