Julius Nyerere Kizimbani
Paperpack

Tamthiliya hii inahusu tukio la kweli la kihistoria lililotokea mwaka 1958. Katika mwaka huo, TANU ikiwa na umri wa miaka minne pekee, serikali ya kikoloni ilidhamiria kuuyumbisha na hatimaye kuusambaratisha kabisa uongozi wa chama. Serikali ya kikoloni ilifanya hivyo kwa kumfikisha Mwalimu Nyerere mahakamani ikimshitaki kuwa: Alikuwa ameishambulia serikali ya Gavana na kuwakashifu na kuwatusi Ma-DC wa Kizungu! Hali hii ilizaa minong’ono ya chini kwa chini na hasira miongoni mwa wananchi kuwa: Iwapo kiongozi wao angepelekwa Ukonga au Isanga, basi wangekuwa tayari kuingia msituni kupigania Uhuru wa Tanganyika kwa mtutu wa bunduki. Baada ya kufanya utafiti wa ndani, mwandishi ametufunulia siri na hila za serikali ya kikoloni za kutaka kuusambaratisha umoja wa Watanganyika na chama cha TANU. Hii ni tamthiliya iliyoandikwa kwa ustadi mkubwa na itawasaidia wasomaji kujua na kuelewa historia hii muhimu ya nchi yetu, Tanzania.

Emmanuel Mbogo

I write about swahili

This book is categorised in
Community Reviews
Book Details
  • ISBN : 9789987871759
  • Publication Date : January 2023
  • Language : Swahili
  • Number of Pages : 63
  • Cover Format : Paperpack
  • Edition : First Edition