
Kamusi hii ya Kiswahili-Kiingereza ina zaidi ya vidahizo 9,000 vya Kiswahili, msamiati linganifu wa Kiingereza na ufafanuzi wake kwa Kiingereza. Pia ina mifano ya matumizi ya vidahizo kwa lugha zote mbili. Kwa sifa hizi, kamusi hii ni kamusi ya kipekee kabisa kwa kuwa na vidahizo na mifano mingi zaidi. Uandaaji wa kazi hii umezingatia wigo na mawanda ya watumiaji wa Kiswahili toka Visiwa vya Zanzibar hadi nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Dhamira ya mchapishaji ni kuwa na kamusi bora itakayomfaa kila mtumiaji na mpenzi wa lugha ya Kiswahili mwenye kuhitaji kufahamu msamiati linganifu wa Kiingereza na matumizi yake mwafaka.
Kamusi hii ni tunu muhimu kwa watumiaji wa kawaida, wanafunzi na wadau wote wa Kiswahili ambao mara kwa mara wana mahitaji ya kutafsiri ama kung’amua maneno na sentensi za Kiswahili kwa lugha ya Kiingereza. Kamusi hii imekusudiwa kuwa mwongozo thabiti wa tafsiri toka lugha ya Kiswahili kwenda Kiingereza kwa matumizi ya jumla ama kitaaluma na kitaalamu.
Kamusi hii ni nyenzo muhimu itakayowawezesha watumiaji wa lugha hizi mbili, hususan wafasiri, wakalimani na wanafunzi kutambua msamiati mahususi wa Kiingereza kwa kila neno la Kiswahili. Kutokana na utajiri mkubwa wa mifano ya matumizi ya vidahizo na msamiati wa lugha zote mbili, kamusi hii itamfundisha mtumiaji kwa wepesi, namna maridhawa na miktadha sahihi ya kutumia maneno ya Kiswahili.
This book is categorised in
- Subjects :
- Reference
No reviews , Be the first to write a review
- ISBN : 9789912752191
- Publication Date : September 2025
- Language : Swahili
- Number of Pages : 604
- Cover Format : Paperpack
- Edition : First Edition