Kichwamaji
Paperpack

Riwaya ya Kichwa Maji ni Riwaya iliyoandikwa mwaka 1974 na E. Kezilahabi. Hii ni Riwaya ya Kisaikolojia kwa sababu inadodosa nafsi ya mhusika, fikra, hisia, mawazo, imani, hofu, mashaka, matumaini na matamanio yake binafsi na athari za mambo hayo kwake na kwa jamii yake. Mwandishi E.Kezilahabi ameeleza mambo mengi yanayohusiana na jina la kitabu chake kwa kubainisha misukosuko na migogoro mbalimbali ambayo imesababisha kupatikana kwa dhamira zinazoendana na Riwaya hii. Riwaya hii yenye vikwazo, ucheshi na kuamsha hisia za wasomaji, imesheheni mbinu lukuki za uandishi ambazo zimependezesha na kuipa Riwaya hii maana kulingana na mazingira au jamii husika. Mwandishi ametanabaisha aina ya Riwaya hii kuwa ni ya Kisaikolojia kwa kutumia wahusika mbalimbali kwenye Riwaya hii. Katika sura ya pili ukurasa wa 30 na 31, ambapo Mzee Kabenga aliiathiri Kisaikolojia familia ya Mzee Mafuru, kwani alifanya matukio ambayo si ya kawaida kwenye jamii kiasi kwamba wanajamii waliathirika kisaikolojia kwa sababu ya mawazo yale.

Euphrase Kezilahabi

Euphrase Kezilahabi alizaliwa Namagondo, Ukerewe, Tanzania, tarehe 13/4/1944. Alisomea katika seminari ya Nyegezi, Mwanza (1957-66) na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alikohitimu mwaka 1970. Alihitimu digrii ya Uzamivu katika Fasihi katika Chuo Kikuu cha Wisconsin, Madison, Marekani, mwaka 1985. Alikuwa Mhadhiri na baadaye Profesa Mshiriki katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye Chuo Kikuu cha Botswana hadi alipougua mwaka 2019. Kezilahabi alifariki tarehe 9/1/2020 na kuzikwa, Namagondo, Ukerewe tarehe 13/1/2020. Mbali na DHIFA, Kezilahabi ameandika vitabu vingine 9, zikiwamo riwaya 6, tamthiliya 1 na diwani 2 za ushairi. Ameandika pia hadithi fupi nyingi.

This book is categorised in
Community Reviews
Related Books
Book Details
  • ISBN : 9789976587012
  • Publication Date : January 2023
  • Language : Swahili
  • Number of Pages : 234
  • Cover Format : Paperpack