
Kiswahili kwa Vitendo Darasa la 4 kinafundisha somo la Kiswahili kulingana na Muhtasari wa somo la Kiswahili Elimu ya Msingi kwa Darasa la 4 wa mwaka 2023. Uandaaji wa kitabu hiki umezingatia misingi na vigezo vya uandishi bora na umelenga kumhamasisha mwanafunzi kupenda kujifunza lugha ya Kiswahili. Kitabu hiki kina hadithi, midahalo na mazoezi mengi. Hivi vyote vinampa mwanafunzi fursa ya kujifunza na kujenga umahiri katika lugha ya Kiswahili. Vipengele vinavyofundishwa katika kitabu hiki ni pamoja na Kusoma, Kuandika, Sarufi, Misamiati, Hadithi fupi, Nahau na Methali. Tuna imani kuwa kitabu hiki kitamjengea mwanafunzi uwezo na kumpa uwanja sahihi wa kujifunza somo la Kiswahili kwa vitendo.
No reviews , Be the first to write a review
- ISBN : 9789912755222
- Publication Date : November 2024
- Language : Swahili
- Number of Pages : 146
- Cover Format : Paperpack
- Edition : First Edition