
Tamthilia hii inaangazia hali ya maisha nchini Tanzania kabla na wakati wa utawala wa Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (Mhe). Tamthilia inaonesha Rais Mwinyi akipokea dola nchi ikiwa inaning’inia katika mtego mkubwa wa kifalsafa, kisiasa na kiuchumi, mtego uliowaweka wananchi katika lindi la taabu na ufukara usiomithilika. Kwa kupitia kisa cha watu wawili walioishi katika zama iliyotangulia na pia katika zama mpya, mwandishi anatujengea taswira ya hali ya mambo katika kipindi hiki na jinsi enzi mpya ilivyoweza kutegua mtego wa zama iliyotangulia na kuwanasua wananchi katika lindi la dhiki na ufukara. Mageuzi anayoyatekeleza Rais Mwinyi katika utawala wake, yanadhihirisha falsafa yake madhubuti ya Li-kulli ajalin kitaab, yaani Kila Zama na Kitabu Chake.
This book is categorised in
No reviews , Be the first to write a review
- ISBN : 9789987871779
- Publication Date : January 2023
- Language : Swahili
- Number of Pages : 115
- Cover Format : Paperpack