Rosa Mistika
Paperpack

Rosa Mistika ni riwaya inayohusu masaibu ya msichana Rosa aliyelelewa katika mazingira ya udhibiti wa kidini na kimila katikati ya lindi la umaskini; na baadaye akakabiliwa na vishawishi pale alipoingia katika shule ya bweni na kisha chuo cha ualimu. Kutokana na malezi aliyoyapata, anashindwa kuvidhibiti vishawishi hivyo na hatimaye anapoteza maisha. Riwaya hiyo inatuingiza katika falsafa ya Kezilahabi kuhusu maisha, Mungu na ubaho ambayo inajitokeza kwa kina na upevu zaidi katika riwaya zake za baadaye.

Euphrase Kezilahabi

Euphrase Kezilahabi alizaliwa Namagondo, Ukerewe, Tanzania, tarehe 13/4/1944. Alisomea katika seminari ya Nyegezi, Mwanza (1957-66) na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alikohitimu mwaka 1970. Alihitimu digrii ya Uzamivu katika Fasihi katika Chuo Kikuu cha Wisconsin, Madison, Marekani, mwaka 1985. Alikuwa Mhadhiri na baadaye Profesa Mshiriki katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye Chuo Kikuu cha Botswana hadi alipougua mwaka 2019. Kezilahabi alifariki tarehe 9/1/2020 na kuzikwa, Namagondo, Ukerewe tarehe 13/1/2020. Mbali na DHIFA, Kezilahabi ameandika vitabu vingine 9, zikiwamo riwaya 6, tamthiliya 1 na diwani 2 za ushairi. Ameandika pia hadithi fupi nyingi.

This book is categorised in
Community Reviews
Related Books
Book Details
  • ISBN : 9789976587111
  • Publication Date : January 2023
  • Language : Swahili
  • Number of Pages : 152
  • Cover Format : Paperpack