Sadaka ya John Okello na Mapinduzi ya Zanzibar
Paperpack

Sadaka ya John Okello ni tamthilia ya kihistoria kuhusu mapinduzi ya tarehe 12/1/1964 visiwani Zanzibar. Wakoloni Waingereza, kabla ya kuondoka visiwani walimkabidhi Sultani Jamshid uhuru na mamlaka ya kuitawala Zanzibar tarehe 01/12/1963. Wazanzibar wengi na hasa Waafrika weusi, waliona kuwa ule ulikuwa uhuru bandia uliokuwa na lengo la kuendeleza usultani, umwinyi na ukandamizwaji. Katikati ya fukuto na taharuki hii, chama cha Afro-Shiraz Party- cha Amani Abed Karume na Umma Party cha Abdulrahaman  Babu, miongoni mwa vyama vingine, viliwahamasisha vijana kushika silaha dhihi ya Usultani. Mtu mmoja, Field Marshall John Okello, kijana mwenye asili ya Uganda, ambaye vitabu vya Historia vimemsahau, alikuwa mstari wa mbele katika kupanga na kutekeleza mapinduzi haya yaliyomng’oa Sultan Jamshid usiku wa kuamkia tarehe 12 Januari 1964. Tamthiliya hii inaangazia nafasi ya harakati za John Okelo katika tukio hili la Kihistoria.

Emmanuel Mbogo

I write about swahili

This book is categorised in
Community Reviews
Book Details
  • ISBN : 9789987871186
  • Publication Date : September 2019
  • Language : Swahili
  • Number of Pages : 68
  • Cover Format : Paperpack
  • Edition : Second Edition