Bibi Pipi na Mawaridi
Paperpack

Mabishano bustanini yalishaanza kupamba moto. Bibi Pipi hakuamini alichokuwa anakisikia. Waridi Pinki alikuwa anapayuka kwa hasira, “Inatosha jamani, acheni huu ujinga!” Waridi Jeupe alikuwa akilia kwa kwikwi huku Waridi Jekundu akiwa ameivimbisha miiba yake tayari kushambulia wakati wowote. Waridi Njano alijawa na hofu na kufunika uso wake kwa mikono yake. Je, inamaanisha chochote mawaridi kuwa na rangi tofauti? Funua kurasa za kitabu hiki na umsadie Bibi Pipi.

Corona Cermak

Corona Kimaro Cermak ni mwandishi wa vitabu vya watoto kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili Anafundisha Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Masaryk kilichopo Cheki na anafundisha Kiingereza watoto wa chekechea. Kwa muda mrefu sasa anatetea na kusimamia utamaduni wa Waswahili katika Jamhuri ya Cheki Yeye pia ni miongoni mwa majaji wa tuzo ya African Teen Writers inayoandaliwa na Writers Space Africa Vitabu vyake Sauti ya Jogoo na Rooster's Voice villipata tuzo ya Mwandishi bora wa mwaka ya Wanawake wenye asili ya Afrika, Ulaya 2019. Kitabu chake Baby Caterpillar kilichapishwa kwenye jarida la Writers Space Africa, toleo la Februari 2022. Anapendelea kusoma na kuandika vitabu. Pia hutumia muda wake mwingi kufundisha na kucheza na watoto.

This book is categorised in
Community Reviews
Related Books
Book Details
  • ISBN : 9789912752108
  • Publication Date : August 2023
  • Language : Swahili
  • Number of Pages : 27
  • Cover Format : Paperpack
  • Edition : Second Edition