Gamba la Nyoka
Paperpack

Gamba la Nyoka ni riwaya inayoonyesha jinsi maamuzi ya kisiasa yasiyotafakariwa yanavyoweza kuwa na athari mbaya kwa wanyonge na wakulima. Ni riwaya inayotashtiti sera zinaoongozwa na ubinafsi, kisasi na pupa ya utekelezaji. Hii ni riwaya inayotumia sitiari na taswira zenye uwezo mkubwa wa kuibua hisia kali na itakayozichokonoa fikira za msomaji hususan kwa namna inavyoupembua unafiki katika matendo ya waja. Hii ni mojawapo wa riwaya bora kabisa kuwahi kuandikwa katika fasihi ya Kiswahili.

Euphrase Kezilahabi

Euphrase Kezilahabi alizaliwa Namagondo, Ukerewe, Tanzania, tarehe 13/4/1944. Alisomea katika seminari ya Nyegezi, Mwanza (1957-66) na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alikohitimu mwaka 1970. Alihitimu digrii ya Uzamivu katika Fasihi katika Chuo Kikuu cha Wisconsin, Madison, Marekani, mwaka 1985. Alikuwa Mhadhiri na baadaye Profesa Mshiriki katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye Chuo Kikuu cha Botswana hadi alipougua mwaka 2019. Kezilahabi alifariki tarehe 9/1/2020 na kuzikwa, Namagondo, Ukerewe tarehe 13/1/2020. Mbali na DHIFA, Kezilahabi ameandika vitabu vingine 9, zikiwamo riwaya 6, tamthiliya 1 na diwani 2 za ushairi. Ameandika pia hadithi fupi nyingi.

This book is categorised in
Community Reviews
Related Books
Book Details
  • ISBN : 9789976587005
  • Publication Date : January 2023
  • Language : Swahili
  • Number of Pages : 192
  • Cover Format : Paperpack