Hidaya ya Shabaan Rober 6
Paperpack

WASIFU WA SITI BINTI SAAD

Riwaya hii ya kiwasifu inazungumzia mwimbaji maarufu wa taarabu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Siti alikuwa mzaliwa wa Fumba kwa wazazi masikini mwishoni mwa karne ya 19. Yeye mwenyewe hakuwahi kusoma elimu rasmi ya darasani. Hata hivyo, aliweza kukwea hadi juu ya kilele cha umaarufu na mafanikio licha ya vikwazo vingi. Aliwezaje? Hiki ni kitabu kinachotia hamasa ya kushinda upinzani mbalimbali hadi kufikia malengo aliyojiwekea mtu.

 

MAISHA YANGU NA BAADA YA MIAKA HAMSINI

Katika riwaya hii ni ya kitawasifu, baba wa fasihi, Shaaban Robert, anasimulia maisha yake katika awamu mbili, yaani kabla ya umri wa miaka hamsini na baada ya miaka hamsini hadi kustaafu kwake. Ndani yake anatufungulia mlango unaotuwezesha kuona machungu na matamu ya maisha yake. Tunaona matarajio na shauku zake, maisha ya uandishi, changamoto alizopitia, falsafa za maisha yake na mafanikio yake katika ajira na familia.

 

MWAFRIKA AIMBA

Hii ni diwani inayosawiri maisha ya mwanadamu. Mshairi ameonesha jinsi maisha yalivyo kwa Mwafrika. Anadokeza dhuluma, manyanyaso, unafiki, usaliti na maovu yanayomkabili. Mwafrika Aimba ni kipaza sauti cha mwandishi katika kufikisha ujumbe kwa hadhira. Amebainisha yale yote yanayomkera Mwafrika pamoja na wajibu wa kila binadamu. Lengo kuu ni kuyafanya maisha ya kila mmoja yawe bora na yenye thamani kubwa hapa duniani.

Shaaban Robert

No

This book is categorised in
Community Reviews
Book Details
  • ISBN : 9789976583663
  • Publication Date : October 2023
  • Language : Swahili
  • Number of Pages : 198
  • Cover Format : Paperpack
  • Edition : First Edition