
Tamthiliya hii inaangazia kisa cha wazazi waliokosa maelewano na mume
kuchukua uamuzi wa kumtaliki mkewe. Japo kutoa talaka ni jambo la mmoja,
madhara yake hakika si jambo linalobaki kwa mmoja pekee. Hatma ya malezi ya
mtoto aliyeachwa na mama aliyetalikiwa na hata ustawi wa familia chini ya mke
mpya ni kamari kubwa ambayo mchezaji hajaweza kuidhania sembuse
kuing’amua. Ndani ya talaka kwa mke imejificha talaka kwa mtoto
inayoambatana na kiza kikubwa. Talaka inamuingiza mtoto katika msitu wa
malezi ya ulimwengu na anapoibuka toka msitu huu mambo yamekwisha
haribika! Si mtu wa kumfaa yeyote tena – si familia yake wala jamii iliyomzunguka.
This book is categorised in
No reviews , Be the first to write a review
- ISBN : 9789912755161
- Publication Date : May 2025
- Language : Swahili
- Number of Pages : 32
- Cover Format : Paperpack
- Edition : First Edition