Mdunguaji
Paperback

Wapiganaji kumi, wakiwemo Watanzania watatu, wanaounda kikosi maalum cha jeshi la Umoja wa Mataifa kilichotumwa kulinda amani nchini Sierra Leone, wanashambuliwa na mdunguaji aliyejificha katika msitu walikokuwamo. Sita kati yao wanauawa, mmoja baada ya mwingine, kwa kudunguliwa na mdunguaji huyo hatari. Ni Mtanzania mmoja tu ndiye anayerudi nchini akiwa hai, huku akirejesha nyumbani miili ya wapiganaji wawili waliouawa na mdunguaji huko Sierra Leone. Miaka mitatu baadaye, mpiganaji aliyeshinda vita vingi vya msituni, Baddi Gobbos, anajikuta akikabiliana na vita vingine katikati ya jiji la Dar pale anapojikuta akiwindwa na wauaji asiowajua. Je, mdunguaji wa Sierra Leone kaingia Tanzania? Wakati huohuo Baddi Gobbos anajikuta akiwa mateka aliyeshindwa katika vita vigumu kuliko vyote alivyowahi kukabiliana navyo maishani mwake... vita vya mapenzi...

"Nimemsoma Tuwa... ama kwa hakika [yeye ni bingwa wa riwaya za taharuki nchini. Mdunguaji ni kali kuliko zote" - Amri Bawji

Hussein Tuwa

I write about swahili

Taarifa za kitabu
  • ISBN : 9789976891928
  • Tarehe ya kuchapishwa : October 2023
  • Lugha : Swahili
  • Idadi ya kurasa : 329
  • Aina ya kava : Paperpack
  • Toleo : First Edition

Jamii ya kitabu hiki ni
Maoni kutoka kwa jamii