Mkimbizi
Paperback

Mwanadada Tigga Mumba anaingia kwenye msukosuko mkubwa maishani, pale anaposhuhudia mauaji ya kutisha akiwa msituni akishiriki utafiti wa mambo ya kale. Maisha yanambadilikia pale anapojikuta akishutumiwa kuwa ni yeye ndiye aliyefanya mauaji yale bila kujitambua, kutokana na maradhi ya akili. Paranoid Schizophrenia!'

Kabla hajajua namna ya kuondokana na shutuma zile, anajikuta akiwindwa kwa chambo na ndoano na wauaji hatari wenye hila lukuki, wakiongozwa na muuaji hatari barani Afrika, The Virus; huku jeshi la polisi nalo likimsaka kwa udi na uvumba kuhusiana na mauaji yale, likiongozwa na mpelelezi mahiri asiyetetereka, Kamishna Msaidizi John Vata.

Mambo yanamzidia ugumu kiasi cha kuutilia mashaka utimamu wa akili yake pale hata watu wake wa karibu wanapomuaminisha kuwa ni kweli amekumbwa na ugonjwa wa akili uliomsukuma kufanya mauaji yale.

Lakini Tigga anaamini kuwa ana siri kubwa na ya hatari, ambayo wote hawaijui - na ili aendelee kuwa hai na hatimaye aibainishe siri hiyo, analazimika kuishi kwa kukimbia huku na huko, akichengana na wauaji hatari, askari waovu, marafiki wa mashaka, huku akikabiliana na mitego ya kikachero.

Anakuwa mkimbizi ndani ya nchi yake. Anayekimbia kwa woga na hofu, huku mahala pekee anapokuwa salama ni peke yake, na mtu pekee anayejihisi salama kuwa naye ni yeye mwenyewe. Peke yake, asiye na kwake... Mkimbizi. "Mkimbizi" ni uthibitisho wa wazi kuwa Hussein Tuwa ndiye bingwa wa taharuki nchini.

Hussein Tuwa

I write about swahili

Taarifa za kitabu
  • ISBN : 9789987971053
  • Tarehe ya kuchapishwa : October 2023
  • Lugha : Swahili
  • Idadi ya kurasa : 357
  • Aina ya kava : Paperpack
  • Toleo : First Edition

Jamii ya kitabu hiki ni
Maoni kutoka kwa jamii