
Habari ya kuuawa kwa mtafiti Grayson Mochiwa haikuwa na sababu ya kumshitua mrembo Zay mpaka pale anapogundua kuwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha kwa rafiki yake kipenzi sio tu hakukuwa kwa bahati mbaya bali pia kulihusiana moja kwa moja na kifo kile kibaya cha mtafiti Grayson Mochiwa.
Zay anajikuta kwenye mtanziko mkubwa pale anapobaini kuwa matukio yale mawili yalikuwa ni sehemu ya mkakati mkubwa wenye usaliti wa kutisha kwa taifa. Je, aweke matumaini yake kwenye vyombo vya dola huku muda wa kumsaka rafikiye ukizidi kumtupa mkono? Au ajitose mwenyewe kumtafuta rafikiye huku akiyaweka rehani maisha yake?
Ni mpaka pale mazingira yanapomkutanisha na askari wawili asiowatarajia, ndipo anaposhuhudia jiji la Dar likifukuta kwa mikabala mizito, mauaji ya kutisha, usaliti usiosemeka na hekaheka zinazoliingiza taifa kwenye machafuko makubwa.
Kwenye MTAFITI, HUSSEIN TUWA anakukutanisha tena -kwa ufupi sana- na John Vata na Tigga Mumba, lakini zaidi anakukutanisha na Inspekta Haroub Kwakwa (unamkubuka?) katika ubora wake.
"Wakati wasomaji, wahakiki, na watafiti wa masuala ya kifasihi na kitamaduni wakiwa wanajiuliza kuhusu uwezo wa mtunzi huyu kuushikilia mwendelezo wa daraja la ubora alilofikia kupitia bunilizi zake zilizotangulia. Tuwa anajitokeza na kujibu kwa vitendo swali hilo. Safari hii anajitokeza kupitia bunilizi hii ya Mtafiti. MTAFITI ni riwaya ya kiyakinifu iliyojaa uchangamfu wa kimatukio (solo) kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho. Athumani S. Ponera (PhD), Mhadhiri wa Taaluma za Kiswahili, UDOM.
- ISBN : 9789987971084
- Tarehe ya kuchapishwa : October 2023
- Lugha : Swahili
- Idadi ya kurasa : 351
- Aina ya kava : Paperpack
- Toleo : First Edition
Jamii ya kitabu hiki ni
- Masomo :
- Swahili
Hakuna maoni , Kuwa wa kwanza kuandika maoni