
Ni mwaka 1891. Mugoha na Nyawelu wametumwa katika kijiji cha mbali ili kumtafutia auni mama yao ambaye anaumwa uchungu wa uzazi. Wakiwa huko nchi ya Uhehe inavamiwa ghafla na majeshi ya Wadachi. Njia ya kurudi nyumbani kupitia bonde la Lugalo imezibwa, lakini inabidi Mugoha na Nyawelu warejee haraka wakiwa na mkunga na taarifa za uvamizi ili kumwokoa Mama na kuinusuru nchi. Je, watafanikiwa kupita katikati ya maadui wakali wenye sura za ajabu na silaha za kutisha ili kutimiza azma hiyo? Fuatana na vijana hao wawili jasiri katika mapambano yao ya usiku ndani ya msitu wa mianzi. Hii ni riwaya fupi ya kihistoria yenye kufikirisha na kusisimua. Inatukumbusha tulikotoka na hivyo kututanabahisha kuhusu huko tuendako.
- ISBN : 9789976587029
- Tarehe ya kuchapishwa : October 2023
- Lugha : Swahili
- Idadi ya kurasa : 54
- Aina ya kava : Paperpack
- Toleo : Second Edition
Jamii ya kitabu hiki ni
- Masomo :
- Swahili
Hakuna maoni , Kuwa wa kwanza kuandika maoni