Sauti ya Jogoo
Paperback

Gundua maisha ya wanyama wa nyumbani. Jifunze kuhusu sauti zao, chakula chao, mahali wanakoishi na pia yupi ni mlafi kupita wengine. Hadithi imepambwa kwa michoro yenye rangi za kuvutia ya aina ya Tingatinga ili watoto wafurahie wakati wanajifunza.

Corona Cermak

Corona Kimaro Cermak ni mwandishi wa vitabu vya watoto kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili Anafundisha Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Masaryk kilichopo Cheki na anafundisha Kiingereza watoto wa chekechea. Kwa muda mrefu sasa anatetea na kusimamia utamaduni wa Waswahili katika Jamhuri ya Cheki Yeye pia ni miongoni mwa majaji wa tuzo ya African Teen Writers inayoandaliwa na Writers Space Africa Vitabu vyake Sauti ya Jogoo na Rooster's Voice villipata tuzo ya Mwandishi bora wa mwaka ya Wanawake wenye asili ya Afrika, Ulaya 2019. Kitabu chake Baby Caterpillar kilichapishwa kwenye jarida la Writers Space Africa, toleo la Februari 2022. Anapendelea kusoma na kuandika vitabu. Pia hutumia muda wake mwingi kufundisha na kucheza na watoto.

Taarifa za kitabu
  • ISBN : 9789912752146
  • Tarehe ya kuchapishwa : August 2023
  • Lugha : Swahili
  • Idadi ya kurasa : 17
  • Aina ya kava : Paperpack
  • Toleo : Second Edition

Jamii ya kitabu hiki ni
Maoni kutoka kwa jamii