FUNGATE YA UHURU
Paperback

Fungate ya Uhuru ni diwani ya mashairi yanayofichua madhila wafanyiwayo
wanyonge na baadhi ya wakubwa, hasa viongozi wanyonyao jasho la wananchi na
kujineemesha migongoni mwa wakulima na wafanyakazi. Mashairi haya yanaonesha
hasira aliyonayo mwandishi kwani “wakubwa” hawa wanaendelea kujistarehesha
huku wakulima na wafanyakazi, ambao ndiyo wajenga nchi, wakiendelea kudidimia
katika lindi la dhiki. Hakika, mashairi haya yatamfanya msomaji atafakari uelekeo
wa nchi yetu na hapohapo kumchokoza atafute ufumbuzi wa “uyabisi” huu!
Kitabu hiki ni tunu kwa wote wapendao ushairi bora na wenyekupenda kutathmini
mwelekeo wa jamii zetu. Vilevile wanafunzi wa fasihi ya Kiswahili shuleni na vyuoni
watanufaika na sanaa ya mwandishi katika ushairi huu yenye vionjo maridhawa.

Muhammed Self Khatibu

Dr. Muhammed Seif Khatib alizaliwa mwaka 1951, Umbuji, Zanzíbar. Alisomea Ualimu katika Chuo cha Nkrumah, Zanzíbar. Mnamo mwaka 1978 alihitimu shahada ya B.A. (Ed.) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kisha alitunukiwa shahada ya uzamili (M.A.) katika Chuo Kikuu cha London (S. O.A .S ) mnamo mwaka 1982. Mwaka 2011 alifaulu shahada ya Uzamivu Chuo Kikuu cha Dodoma. Aidha yeye ni mtunzi maarufu wa makala na vitabu kadhaa vya ushairi wa Kiswahili kama vile: Ukombozi wa Zanzíbar (OUP 1975 ); Pambazuko la Afrika (E.A.P 1982), Taarabu Zanzíbar (T.P.H. 1992), Wasakatonge (OUP, 2003), Chanjo( TUKI, 2014) na Vifaru Weusi (Vide-Muwa, 2016). Mwandishi amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alishawhi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo katika Serikali ya awamu ya nne. Kwa sasa Dr. Muhammed Seif Khatib ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar.

Book Details
  • ISBN : 9789987871124
  • Publication date : February 2019
  • Language : Swahili
  • Number of Pages : 55
  • Cover Format : Paperback
  • Edition : Third Edition

This book is categories in
Community Reviews