
Fungate ya Uhuru ni diwani ya mashairi yanayofichua madhila wafanyiwayo
wanyonge na baadhi ya wakubwa, hasa viongozi wanyonyao jasho la wananchi na
kujineemesha migongoni mwa wakulima na wafanyakazi. Mashairi haya yanaonesha
hasira aliyonayo mwandishi kwani “wakubwa” hawa wanaendelea kujistarehesha
huku wakulima na wafanyakazi, ambao ndiyo wajenga nchi, wakiendelea kudidimia
katika lindi la dhiki. Hakika, mashairi haya yatamfanya msomaji atafakari uelekeo
wa nchi yetu na hapohapo kumchokoza atafute ufumbuzi wa “uyabisi” huu!
Kitabu hiki ni tunu kwa wote wapendao ushairi bora na wenyekupenda kutathmini
mwelekeo wa jamii zetu. Vilevile wanafunzi wa fasihi ya Kiswahili shuleni na vyuoni
watanufaika na sanaa ya mwandishi katika ushairi huu yenye vionjo maridhawa.
No reviews , Be the first to write a review
- ISBN : 9789987871124
- Publication Date : February 2019
- Language : Swahili
- Number of Pages : 55
- Cover Format : Paperpack
- Edition : Third Edition