HARUSI
Paperback

Vigelegele, vi?ijo na cherekochereko za kina mama wakiimba mamie mwana so ukaule
mgeni kengia ndizo zinazokamilisha kilele cha harusi ya Rahman, mtoto wa Alhaj Mwinyi
Karim kwa Shufaa binti wa Mwinyi Sitaki Shari.
Hakuna kinachokosekana siku hiyo. Fahari yote na utajiri wa Alhaj Karim ulitengwa
kukamilisha ndoa hiyo ili iwe harusi ya kusimuliwa. Ama kweli watu waliohudhuria
walifurahi na kukubaliana kuwa, Rahman bin Mwinyi kapata; sio kama kakaye, Dakta
Mustafa, ambaye hakua?ikiana na wazazi wake kwenye kuchagua mke.
Lakini ni kweli kwamba Rahman kapata mke “mtoto wa watu” au ni kama mkwezi mmoja
kwenye karamu kubwa ya maulid ya harusi anavyojibu kwa dharau, “harusi za siku hizi
harusi?”
Harusi si riwaya tu bali ni kielelezo cha mila na desturi za jamii ya watu wa mwambao wa
pwani ya Afrika Mashariki. Ni wazi kuwa wasomaji wengi watafurahiwa na riwaya hii.
Abdallah J. Saffari ni mtunzi nguli wa riwaya na tamthiliya za kiswahili. Kati ya kazi zake
maarufu ni Kabwela (Longman:1980, APE Network 2018) na Joka la Mdimu (HUDA: 2007,
APE Network: 2017). Riwaya zake nyingine, Njia Panda na Makombo ya Halua, ziko njiani.

Abdallah Saffari

Abdallah J. Saffari ni mtunzi nguli wa riwaya na tamthiliya za kiswahili. Kati ya kazi zake maarufu ni Kabwela (Longman:1980, APE Network 2018) na Joka la Mdimu (HUDA: 2007, APE Network: 2017). Riwaya zake nyingine, Njia Panda na Makombo ya Halua, ziko njiani.

Book Details
  • ISBN : 97899877016981
  • Publication date : December 2017
  • Language : Swahili
  • Number of Pages : 200
  • Cover Format : Paperback
  • Edition : First Edition

This book is categories in
Community Reviews
Related Books