JOKA LA MDIMU
Paperback

Tino alistakimu Kiungani Sega, nje kidogo ya jiji la Mindule. Alibangaiza kwa kuvuta
kwama. Alikuwa na mke na watoto watatu. Mtoto wake mkubwa, Cheche (mvulana wa
miaka 12) gha?la alivunjika kiuno katika michezo maalumu ya kusherehekea uhuru wa
nchi yao. Baada ya kusota katika hospitali ya wilaya hali yake ilizidi kuzorota. Iliendelea
hivyo hata pale alipoonana na Dakta Mikwala, bingwa wa mifupa katika hospitali kuu ya
taifa jijini Mindule.
Kutokana na juhudi za Amani, sahibu yake Tino ambaye alikuwa dereva wa teksi jijini
Mindule, Dakta Mikwala alipendekeza Cheche akatibiwe upesi katika hospitali mahsusi ya
mifupa ya Glasgow, Uingereza ama sivyo Cheche angekuwa kiwete maisha yake yote.
Sakata likawa kupata kibali cha kununua pesa za kigeni za matibabu na safari. Yote tisa,
kumi ilibaki namna ya kuzipata pesa zenyewe!
Hadithi hii ni kielezeo cha matatizo makubwa ya kisiasa na uchumi yanayozikumba nchi
nyingi zinazoendelea hususan Afrika. Inafaa sana kusomwa na wapenzi wa fasihi wa aina
na daraja zote.

 

Abdallah Saffari

Abdallah J. Saffari ni mtunzi nguli wa riwaya na tamthiliya za kiswahili. Kati ya kazi zake maarufu ni Kabwela (Longman:1980, APE Network 2018) na Joka la Mdimu (HUDA: 2007, APE Network: 2017). Riwaya zake nyingine, Njia Panda na Makombo ya Halua, ziko njiani.

Book Details
  • ISBN : A9789987701698
  • Publication date : October 2017
  • Language : Swahili
  • Number of Pages : 160
  • Cover Format : Paperback
  • Edition : First Edition

This book is categories in
Community Reviews
Related Books