Pepo ya Mabwege
Paperpack

Pepo ya Mabwege ni riwaya ya kitashtiti inayoangazia mazingira ya kisiasa, kijamii na kiuchumi barani Afrika katika miaka ya 1960 na 1970, baada ya vuguvugu la kudai uhuru na uongozi wa dola kutulia. Changamoto mpya ziliibuka na kutishia kuzamisha ndoto za uhuru zilizobeba matumaini ya wengi. Josina na Kalenga wanajifunga kibwebwe kupambana na ulaghai na ufisadi uliokithiri kwenye ngazi za juu za uongozi katika serikali mpya ya wazawa inayojibainisha kuwa serikali ya watu.

Harrison Mwakyembe

Dk. Harrison G. Mwakyembe amekuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, na Waziri wa Wizara mbalimbali katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia, Dk. Mwakyembe ni mdau kindakindaki wa lugha ya Kiswahili anayetambuliwa na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kama Mwalimu wa kufundisha Kiswahili kwa Wageni kuanzia Septemba, 2018.

This book is categorised in
Community Reviews
Related Books
Book Details
  • ISBN : 9789912752177
  • Publication Date : October 2023
  • Language : Swahili
  • Number of Pages : 268
  • Cover Format : Paperpack
  • Edition : Fourth Edition