Takadini
Paperpack

Riwaya ya kipeke inayovutia hisia, ambayo inasawiri mila na desturi huku ikijikita katika karne ya 19 nchini Zimbabwe. Japokuwa ilikuwa ni mwiko kuruhusu kuwepo kwa mazeruzeru, yaani wakipokonywa maisha yao punde wazaliwapo, mwanamke mmoja jasiri anamtorosha takadini, mwanawe aliye zeruzeru ili kuyanusuru maisha yake.

Lakini, hata katika nchi wanayokimbilia, jamii inavutana sana, wengi wakiamini kuwa kuwepo kwa Takadini na mama yake kungewaletea mkosi. Hata hivyo, baadhi ya wazee wanatumia busara kuupoza mgogoro huo, japokuwa kwa vikwazo vingi.

Takadini alikuwa sope yaani zeruzeru na hatimaye alipata ulemavu, akatengwa na watoto wenzake huku wengine wakimkejeli. katikati ya unyonge na mashaka, Takadini na mama yake wanafarijika kwa mapenzi wanayopewa na Baba Chivero, mganga mshauri ambaye kabla hajafa anamfundisha Takadini tiba mbalimbali. Hata Takadini anapoibuka kuwa mpigaji mbira hodari, hatimaye jamii inaanza kuvutiwa naye. Akatokea msichana akampenda, wakaoana na wakapata mtoto asiye sope. Kumbe ulemavu wake na uzeruzeru wake, havikumzuia kuyatenda yale wafanyayo binaadamu wengine. Je, taswira hiyo ya mila dhidi ya masope ingepokewaje na jamii ya mama yake Takadinii pindi watakaporeje?  jipatie riwaya hii ya kusisimua kupitia www.apenetwork.org

Ben J. Hanson

Ben J Hanson pamoja na Islyn, mkewe, awali walikuwa raia wa Jamaica ambao tangu mwaka 1981, wamehamia rasmi nchini Zimbabwe. Ndiye mwandishi wa jarida la vijana, the new Generation. Kazi zake ambazo tayari zimechapishwa ni Just Feelings, mkusanyiko wake wa kwanza wa mashairi, pamoja na vitabu vya watoto: Dont swim in River Gwai, Sekuru's Journey by Air na Elephant on a while.

This book is categorised in
Community Reviews
Related Books
Book Details
  • ISBN : 9789987602193
  • Publication Date : December 2016
  • Language : Swahili
  • Number of Pages : 102
  • Cover Format : Paperpack
  • Edition : First Edition