Dhifa
Paperback

Dhifa ni diwani ya mwisho ya Kezilahabi. Diwani hii inakusanya tungo za miaka ya 1990-2008, wakati wa mageuzi ya kiliberali mamboleo yaliyoasisiwa na Rais Ali Hassan Mwinyi na kuendelezwa na warithi wake baada ya Mwalimu J.K. Nyerere kustaafu. Jina la diwani linaakisi wazo lake kuu: “Dhifa” – yaani sherehe ya kujinufaisha baada ubinafsishaji na uporaji wa mali na rasilimali za Umma. Jina la diwani hii linabeba motifu kuu ya kipindi hicho: ufisadi na ubadhirifu uliokithiri.

Euphrase Kezilahabi

Euphrase Kezilahabi alizaliwa Namagondo, Ukerewe, Tanzania, tarehe 13/4/1944. Alisomea katika seminari ya Nyegezi, Mwanza (1957-66) na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alikohitimu mwaka 1970. Alihitimu digrii ya Uzamivu katika Fasihi katika Chuo Kikuu cha Wisconsin, Madison, Marekani, mwaka 1985. Alikuwa Mhadhiri na baadaye Profesa Mshiriki katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye Chuo Kikuu cha Botswana hadi alipougua mwaka 2019. Kezilahabi alifariki tarehe 9/1/2020 na kuzikwa, Namagondo, Ukerewe tarehe 13/1/2020. Mbali na DHIFA, Kezilahabi ameandika vitabu vingine 9, zikiwamo riwaya 6, tamthiliya 1 na diwani 2 za ushairi. Ameandika pia hadithi fupi nyingi.

Taarifa za kitabu
  • ISBN : 9789976587074
  • Tarehe ya kuchapishwa : October 2022
  • Lugha : Swahili
  • Idadi ya kurasa : 67
  • Aina ya kava : Softcover
  • Toleo : First Edition

Jamii ya kitabu hiki ni
Maoni kutoka kwa jamii