
Tamthilia hii fupi ina kisa cha kustaajabisha na kinachoangazia suala
linalojitokeza pale ambapo wanajamii wanapokuwa radhi kushinikiza wengine
kuishi katika hofu ili tu hadhi yao katika jamii isipotee. Heshima ya mtu mmoja
ilindwe kwa kudhalilisha na kuonea wengine kama vile nao hawana heshima
inayopaswa kulindwa na mioyo inayojali hadhi. Mzee Issa anawakilisha baadhi
ya wanaume katika jamii ambao vitendo vyao vimewavunjia heshima na hadhi
wengine shinikizo na vitisho, jamii inawaona kuwa wenye hadhi huku wale
wanaoonewa wanonekana ndio wasio na heshima. Hii ni kati ya tamthiliya bora
kabisa ambayo inakosoa mfumo dume si katika jamii pekee, bali katika fikra na
kuamrisha uwajibikaji katika kulinda heshima ya wote na si ya baadhi ya watu.
- ISBN : 9789912755154
- Tarehe ya kuchapishwa : May 2025
- Lugha : Swahili
- Idadi ya kurasa : 24
- Aina ya kava : Paperpack
- Toleo : First Edition
Jamii ya kitabu hiki ni
Hakuna maoni , Kuwa wa kwanza kuandika maoni