Karibu Ndani
Paperback

Karibu ndani ni diwani ya pili ya Kezilahabi. Hii imekusanya mashairi yaliyohusu harakati za Ujamaa nchini Tanzania, hususani “kushindwa” kwa Ujamaa kutokana na unjozi na upofu wa waasisi wake; mgogoro wa ushairi wa miaka ya 1970 kati ya wanajadi na wanamabadiliko, tafakuri kuhusu maisha ya kawaida, na kuhusu falsafa. Falsafa ya Kezilahabi kuhusu maisha na ulimwengu iliyomo katika kazi zilizotangulia bado inajitokeza katika diwani hii.

Euphrase Kezilahabi

Euphrase Kezilahabi alizaliwa Namagondo, Ukerewe, Tanzania, tarehe 13/4/1944. Alisomea katika seminari ya Nyegezi, Mwanza (1957-66) na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alikohitimu mwaka 1970. Alihitimu digrii ya Uzamivu katika Fasihi katika Chuo Kikuu cha Wisconsin, Madison, Marekani, mwaka 1985. Alikuwa Mhadhiri na baadaye Profesa Mshiriki katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye Chuo Kikuu cha Botswana hadi alipougua mwaka 2019. Kezilahabi alifariki tarehe 9/1/2020 na kuzikwa, Namagondo, Ukerewe tarehe 13/1/2020. Mbali na DHIFA, Kezilahabi ameandika vitabu vingine 9, zikiwamo riwaya 6, tamthiliya 1 na diwani 2 za ushairi. Ameandika pia hadithi fupi nyingi.

Taarifa za kitabu
  • ISBN : 9789976587104
  • Tarehe ya kuchapishwa : January 2023
  • Lugha : Swahili
  • Idadi ya kurasa : 49
  • Aina ya kava : Paperpack

Jamii ya kitabu hiki ni
Maoni kutoka kwa jamii