Kichomi
Paperback

Kichomi ni diwani inayoakisi mawazo anuwai kutoka kwenye nyanja tofauti za maisha, kama vile uchumi, siasa, utamaduni, ndoa na dini; hususan katika sehemu ya kwanza ya diwani aliyoiita Mashairi ya Mwanzo. Je, ni mawazo gani hayo? Katika sehemu ya pili ya diwani hii aliyoiita Fungueni Mlango, mshairi ameibua swali muhimu linalousakama moyo wake: Maana ya maisha ni nini? Hii ni diwani chokonozi iliyojaa tafakuri zisizoepukika katika maisha yetu.

Euphrase Kezilahabi

Euphrase Kezilahabi alizaliwa Namagondo, Ukerewe, Tanzania, tarehe 13/4/1944. Alisomea katika seminari ya Nyegezi, Mwanza (1957-66) na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alikohitimu mwaka 1970. Alihitimu digrii ya Uzamivu katika Fasihi katika Chuo Kikuu cha Wisconsin, Madison, Marekani, mwaka 1985. Alikuwa Mhadhiri na baadaye Profesa Mshiriki katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye Chuo Kikuu cha Botswana hadi alipougua mwaka 2019. Kezilahabi alifariki tarehe 9/1/2020 na kuzikwa, Namagondo, Ukerewe tarehe 13/1/2020. Mbali na DHIFA, Kezilahabi ameandika vitabu vingine 9, zikiwamo riwaya 6, tamthiliya 1 na diwani 2 za ushairi. Ameandika pia hadithi fupi nyingi.

Taarifa za kitabu
  • ISBN : 9789976583724
  • Tarehe ya kuchapishwa : June 2024
  • Lugha : Swahili
  • Idadi ya kurasa : 330
  • Aina ya kava : Paperpack

Jamii ya kitabu hiki ni
Maoni kutoka kwa jamii