
Alex ni afisa usalama, anapenyezwa Wizara ya Madini kung’amua kinachoendelea katika upotevu tata wa mapato ya Taifa ndani ya biashara ya madini ya Tanzanite. Anaambulia taarifa kiduchu. Kitendawili kinabaki, ni kina nani wanahusika kwenye biashara hii haramu kimataifa? Kutegua kitendawili, Alex anaondolewa wizarani ili kutumwa kwenye misheni ya siri ili kung’amua mtandao na hatimaye Taifa liweze kuudhibiti Uchochoro mzima wa Tanzanite. Anakutana na mauaji, usaliti, visasi na ukatili toka kwa magenge ya wahalifu ya kimataifa.
- ISBN : 9789976583892
- Tarehe ya kuchapishwa : June 2023
- Lugha : Swahili
- Idadi ya kurasa : 288
- Aina ya kava : Paperpack
- Toleo : First Edition
Jamii ya kitabu hiki ni
- Masomo :
- Swahili
Hakuna maoni , Kuwa wa kwanza kuandika maoni