Dunia Uwanja wa Fujo
Paperpack

“Dunia uwanja wa fujo” inaelezea jinsi maisha yaliyopo duniani ni sawa sawa na fujo kwani kila mtu anayekuja duniani huleta fujo zake na baadae kutoweka. Mwandishi E. Kezilahabi anaelezea katika jamii kila mtu anakuja duniani kufanya fujo zake na kusababisha matatizo mbalimbali katika jamii yake kama vile mauaji, ukabila, umalaya, uchawi, ubakaji ulevi wa kupindukia nk. hivyo basi mwandishi anaamini kwamba katika dunia kila mtu anakuja na fujo zake na kutoweka, mfano mhusika Tumaini katika Riwaya hii ameleta fujo zake kama vile umalaya,  mauaji na mengine mengi na baadae kutoweka.

Euphrase Kezilahabi

Euphrase Kezilahabi alizaliwa Namagondo, Ukerewe, Tanzania, tarehe 13/4/1944. Alisomea katika seminari ya Nyegezi, Mwanza (1957-66) na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alikohitimu mwaka 1970. Alihitimu digrii ya Uzamivu katika Fasihi katika Chuo Kikuu cha Wisconsin, Madison, Marekani, mwaka 1985. Alikuwa Mhadhiri na baadaye Profesa Mshiriki katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye Chuo Kikuu cha Botswana hadi alipougua mwaka 2019. Kezilahabi alifariki tarehe 9/1/2020 na kuzikwa, Namagondo, Ukerewe tarehe 13/1/2020. Mbali na DHIFA, Kezilahabi ameandika vitabu vingine 9, zikiwamo riwaya 6, tamthiliya 1 na diwani 2 za ushairi. Ameandika pia hadithi fupi nyingi.

This book is categorised in
Community Reviews
Related Books
Book Details
  • ISBN : 9789976587043
  • Publication Date : January 2023
  • Language : Swahili
  • Number of Pages : 233
  • Cover Format : Paperpack