Hidaya ya Shaaban Robert 5
Paperback

PAMBO LA LUGHA
Huu ni mkusanyiko wa mashairi ya Shaaban Robert unaoakisi maisha ya jamii kwa kuangazia nyanja mbalimbali na mabadiliko yake. Diwani hii pendwa imedhihirisha umaarufu na utamu wake kwa kutajwa na kunukuliwa katika majukwaa mbalimbali ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Pambo la Lugha ni kitabu kilichopambwa si kwa dhamira na ujumbe tu, bali pia kwa mitindo inayovutia jicho la msomaji na kuibua tafakuri za msingi za maisha ya mwanadamu.

MASHAIRI YA SHAABAN ROBERT
Hii ni moja ya diwani fupi miongoni mwa kazi za Shaabab Robert inayozungumzia namna bora ya wanajamii kuwa na mahusiano bora na kujiletea maendeleo. Masuala mbalimbali kama vile dini, maadili na maisha kwa jumla yanazungumziwa humu na mwandishi. Chachu hii inaleta changamoto ya kujitahidi kupambana hadi kufikia malengo ya maisha bora ambayo ni ndoto ya kila mmoja. Hakika dafina ya maisha iliyofichwa inafichuliwa katika diwani hii tayari kwa yeyote atakayeisoma.


TENZI ZA MARUDI MEMA NA OMAR KHAYYAM
Utungo huu umejaa tunu na mafunzo kwa jamii ukisawiri mwelekeo wa jamii kwa kutoa miongozo inayoweza kutumika kama reli za maisha ya kila siku. Marudi si marudi tu, bali yapaswa kuwa marudi mema yatakayokuwa msaada kwa jamii. Ungana na mtunzi ili kufaidi kazi hii yenye msisimko wa pekee unaoambatana na elimu mujarab kwa jamii.

Shaaban Robert

No

Taarifa za kitabu
  • ISBN : 9789976583656
  • Tarehe ya kuchapishwa : October 2023
  • Lugha : Swahili
  • Idadi ya kurasa : 235
  • Aina ya kava : Paperpack
  • Toleo : First Edition

Jamii ya kitabu hiki ni
Maoni kutoka kwa jamii